Uchaguzi wa Katibu Mkuu wa OIF waahirishwa kwa mwaka mmoja, Mushikiwabo aendelea kubaki madarakani
Uchaguzi wa Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) uliofanyika katika mkutano wa 20 wa Francophonie mjini Phnom Penh, nchini Cambodia, umeahirishwa kwa mwaka mmoja baada ya nchi wanachama kushindwa kufikia mwafaka kuhusu mgombea atakayeongoza shirika hilo kwa kipindi cha 2027–2030.