Mkurugenzi wa zamani wa kituo cha watu wenye ulemavu nchini Rwanda akamatwa
Zaidi ya miaka thelathini baada ya matukio hayo, mwanadini wa zamani wa Rwanda amekamatwa nchini Ubelgiji, akishukiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi, "kwa kufanya ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu, haswa uhalifu wa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu, nchini Rwanda," kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa shirikisho la Ubelgiji.