Afrika Kusini: Watu wanaoshukiwa kuajiriwa kupigana nchini Ukraine wakamatwa
South Africa: People wanted for hiring to fight in Ukraine arrested
Polisi ya Afrika Kusini imetangaza leo Jumatatu, Novemba 9, kukamatwa kwa raia tisa wa Zimbabwe wanaoshukiwa kuwa na nia ya kwenda kupigana katika safu ya jeshi la Urusi nchiniUkraine. Operesheni hii ilifanywa kwa kuzingatia uchunguzi uliofanywa na Interpol na mashirika mengine ya ndani na kimataifa, kwani raia wa Afrika wamekuwa wakilengwa tangu mwanzo wa vita kwa kampeni za kuajiri zinazolenga kuwaandikisha katika jeshi la Urusi.