Watu saba hawajulikani waliko baada ya jengo kuporomoka Eastleigh
Watu saba bado hawajulikani waliko baada ya jengo la ghorofa 18 kuporomoka Eastleigh, Nairobi, huku shughuli za uokoaji zikiendelea kwa tahadhari kutokana na hofu ya kuathiri hewa inayoweza kuwasaidia manusura walio chini ya vifusi. Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen alisema wafanyakazi 67 waliokuwa wakijenga jengo hilo kando ya 9th Street kabla ya kuporomoka wamepatikana. Mmoja alijeruhiwa huku wengine 66 wakinusurika bila majeraha. Hata hivyo, watu saba…